Mama, Bintiye Watorokwa na Wapenzi kwa Kujifungua Watoto Wenye Ulemavu

Hakuna mzazi mwenye upendo anayetumaini na kusali kupata mtoto mwenye ulemavu wa kimwili au kiakili anapozaliwa


Matukio ya kusikitisha yanapotokea, wanandoa wanahitaji kushikamana ili kupeana upendo na utegemezo. Mama mmoja ameeleza kisa chake cha kukataliwa na mumewe baada ya kujifungua mtoto mwenye matatizo ya kimwili. Millicent Mahero kutoka Donholm, Nairobi, aliambia TUKO.co.ke bintiye ambaye pia alijifungua mtoto mwenye ulemavu pia aliachwa na mpenzi wake.


"Ninaishi na mwanangu, Derrick, ambaye ana ugonjwa wa mishipa ya fahamu ambao umemfanya awe na kifafa. Pia ninaishi na mjukuu wangu wa kike mwenye umri wa miaka mitano anayeishi na ugonjwa wa kupooza kwa ubongo," alisema. Derrick, kifungua mimba wake, ndiyo sababu aliacha ndoa yake baada ya baba yake kumkataa kwakufuatia hali yake. Licha ya changamoto za maisha, ilimbidi ajitie moyo kwa sababu ya mtoto wake ambaye hajawahi kuwa na babake tangu azaliwe. "Nilichukua muda mwingi kujifungua na hilo lilimuathiri mtoto wangu wakiume Derrick. 


Mmabo hayajakuwa rahisi kwetu sisi tangu tulipotengana na mume wangu," alisimulia. Akiwa bado anahangaika kumtunza mwanawe, akiuguza jeraha la huzuni na kukataliwa na mpenzi wake, bintiye Catherine Baraza pia alipata ujauzito. "Alijifungua mtoto ambaye alipata jeraha la ubongo lililosababisha ugonjwa wa kupooza kwa ubongo," alisimulia. Baba ya mtoto alimwacha Baraza, kwa vile mama yake alikuwa amekataliwa kwa uchungu na mpenzi wake.


Mahero alisema mkwe huyo mtarajiwa alitoroka kutokana na "aibu" ya kupata mtoto mwenye ugonjwa wa kupooza kwa ubongo. Hata hivyo, bintiye Baraza baadaye aliolewa na mwanamume mwingine na kumwacha mtoto wake chini ya uangalizi wa mamake, Mahero. Kama bibi mwenye upendo ambaye anaelewa uchungu wote, Mahero alianza kumtunza mtoto huyo kwa upendo. Mzigo ni mzito sana hivi kwamba anaanguka katika msongo wa mawazo mara kadhaa na anaugua ugonjwa wa uabisi na shinikizo la damu.

Chanzo: TUKO.co.ke


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo