Barobaro mmoja kutoka Nigeria kwenye Twitter, Sir Fresh, amesimulia tukio lake la kuhuzunisha na mpenzi wake wa muda mrefu aliyemtoroka.
Sir Fresh alifichua jinsi alivyomfadhili msichana huyo kupitia shule kutokana na upendo wake wa dhati. Cha kusikitisha ni kwamba, licha ya jitihada zake zote za kuonyesha mapenzi yake, mrembo huyo alimwacha na kuhepuka na mwanamume mwingine. Kulingana na mwanamume huyo aliyevunjika moyo, amekuwa na huzuni tangu alipotupwa.
Sir Fresh alilia kwenye Twitter, akisema kwamba haoni kama kuwa maana ya kuishi tena, jambo lililowafanya watyu mitandaoni kumuonea huruma. Ujumbe wake ulisema; "Baada ya kumfadhili binti huyu shuleni aliniacha na kwenda kwa mwanaume mwingine. Huyu ndiye msichana yule yule niliyemnunulia gari mwaka jana, nimevunjika moyo kwa huzuni, siwezi kula wala kulala. Nimekuwa nikilia tangu nilipofahamu nimeachwa. Nimechoka na maisha haya. Sioni haja ya kuishi tena."