Mwanaume mmoja amemshangaza mamake kwa kumpa zawadi ya nyumba ya kifahari, miaka tisa baada ya kudhihakiwa na kutuowa nje na mtoto wake wa kambo kufuatia kifo cha mumewe.
Kabla ya kumpa mama zawadi hiyo, jamaa alikuwa amemwambia mamake kakake mkubwa alikiwa amenunua shamba na kwamba walitaka azuru eneo hilo.
Alipofika huko, alikabidhiwa ufunguo wa nyumba nzima. Video ya TikTok iliyonasa tukio hilo la kufurahisha ilionyesha jinsi mwanamke huyo alivyobaki kinywa wazi akizipokea funguo hizo. Aliingia mahali hapo na mara akajumuika na bintiye ambaye alijibwaga sakafuni kutokana na msisimko.