Mabaki ya mwili wa mtoto Emanuel Marco Nyangela aliyefariki dunia kwa kuliwa na fisi yamezikwa kijijini kwao Mwangika wilayani Kwimba mkoani Mwanza
Tukio hilo lilitokea Desemba 27,2022 saa 12 jioni kijijini hapo baada ya mtoto huyo kunyakuliwa na fisi na kutokomea naye kuelekea msituni
Baadhi ya mabaki yaliyopatikana katika eneo la tukio ni fuvu la kichwa, ubongo, nguo alizokuwa amevaa pamoja na meno mawili.