Mkulima mmoja kutoka Uganda ambaye ana watoto 102 na wajukuu 568 aliowazaa na wake 12 hatimaye ameamua kupanua zaidi familia yake.
Musa Hasahya mwenye umri wa miaka sitini na saba sasa amewataka wake zake kutumia vidonge vya kupanga uzazi ili waweze kumudu kununua chakula cha familia.
Daily Mail iliripoti kuwa Musa alidai mshahara wake umekuwa ukipungua kila mwaka na kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha huku familia yake ikizidi kuongezeka.
Nilioa mwanamke mmoja baada ya mwingine. Mwanaume anawezaje kuridhika na mwanamke mmoja," gazeti la The Sun lilimnukuu.
Hasahya na familia yake wanaishi Lusaka nchini Uganda ambapo ndoa za wake wengi ni halali, lakini njia za uzazi wa mpango zina utata na mara nyingi huhusishwa na uasherati. Mkewe mdogo, Zulaika, mama wa watoto wake 11, alisema: "Sitaki watoto wengine. Hali ya kifedha imekuwa ngumu hapa lazima tupange uzazi."
Takriban thuluthi moja ya watoto wa Musa wanaishi naye kwenye shamba lake. Kitinda mimba wake ana umri wa miaka sita na kifungua mimba miaka 51 - karibu miaka 20 zaidi kuliko Zulaika. Hawezi tena kufanya kazi kwa sababu ya afya mbaya, na wawili kati ya wake zake wameondoka kwa sababu ya changamoto za kifedha. Alisema kuwa wake zake wote wanaishi nyumba moja ili awachunge waepuke kutoroka na wanaume wengine.
Hasahya, ambaye anaaminika kuwa mwanamume mwenye wake wengi zaidi katika Wilaya ya Butaleja, aliiomba serikali inayoongozwa na Yoweri Museveni kusaidia katika kutunza familia yake kubwa kwani uchumi umekuwa mgumu.