Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Makete
mkoani Njombe hii leo kwa kauli moja limepitisha mapendekezo na marekebisho ya
bajeti ya mwaka ujao wa fedha 2017/2018
Katika kikao cha baraza hilo kilichofanyika kwenye ukumbi
wa halmashauri hiyo, baada ya bajeti hiyo kuwasilishwa, wamepata nafasi ya
kuchangia na kutoa mapendekezo yao kabla ya kuipitisha
Awali akizungumza katika baraza hilo Mkuu wa wilaya ya
Makete Mh Veronica Kessy amegusia baadhi ya maeneo ambayo yameonekana yana
changamoto kidogo na kuliomba baraza hilo kutilia mkazo maeneo hayo ikiwemo
urejeshaji wa fedha za mfuko wa vijana na wanawake, Maeneo ya yote ya serikali
kupimwa na kuwa na hatimiliki pamoja na kuwepo kwa mgawanyo sawa wa miradi ya
maendeleo katika wilaya nzima bila kuwepo na upendeleo wa maeneo fulani
Naye mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh
Egnatio Mtawa akizungumza katika baraza hilo mbali na kuomba ushirikiano wa
kimaendeleo kwa waheshimiwa madiwani wote, lakini amesisitiza umuhimu wa kutoa
shukurani na kusifia serikali pale inapofanya mambo mazuri ya kimaendeleo
badala ya kuishia kutoa changamoto pekee
Mapendekezo hayo ya bajeti yamepitishwa ikiwa imesalia
miezi 6 pekee kumaliza mwaka huu wa fedha 2016/2017 kabla ya kuingia mwaka
mwingine wa fedha wa serikali ambao utatekelezwa ndani ya mapendekezo hayo
baada ya kuwa bajeti rasmi

Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete wakiwa kwenye baraza la kupitisha mapendekezo ya bajeti ya mwaka ujao wa fedha 2017/2018 yaliyofanyika leo 11.01.2017 katika Ukumbi wa halmashauri hiyo. Bajeti hiyo imepitishwa na wajumbe wote wa baraza hilo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh Egnatio Mtawa akiendesha baraza hilo hii leo
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessy akizungumza machache katika baraza hilo hii leo