MTOTO ADAIWA KUUAWA KWA KIPIGO NA BABA YAKE MZAZI

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi ACP Dhahiri Kidavashari
******
JESHI la Polisi Wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, linamtafuta mkazi wa Malangali, Bw. Saimon Paskali kwa kosa la kuwapiga watoto wake, kumuua mmoja na kukimbia kusikojulikana.
 
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana baada ya mtuhumiwa kurudi nyumbani akitokea kwenye Sherehe ya Komonio akiwa amelewa na kuanza kuwapiga watoto wake kwa fimbo hadi wakazirai.
 
Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Frednandi Rwegasila, alisema mtuhumiwa alikuwa akiishi na watoto muda mrefu baada ya kuachana na mkewe.
 
Aliwataja watoto hao kuwa ni Daniel Paskali (11) ambaye ndiye aliyefariki na Jackson Paskali (9) ambao baada ya kuzirai kwa kipigo na mtuhumiwa kukimbia, majirani walikwenda kutoa msaada wa kuwapeleka hospitali.
 
"Wakiwa njiani, Daniel alifariki dunia wakati Jackson amelazwa katika Hospitali ya Mkoa akiendelea kupatiwa matibabu na ameumizwa sehemu mbalimbali ya mwili wake," alisema.
 
Kamanda Rwegasila alisema jeshi hilo linaendelea kumsaka mtuhumiwa ili aweze kufikishwa mahakamani.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo