Mungu Hakuruhusu Yesu Kulelewa na Mama Singo, Lindeni Ndoa - Mchungaji

Mhubiri wa Tanzania Tony Kapola amewashauri wanandoa kuziba ufa badala ya kujenga ukuta, na waepukane na ndoa zao kusambaratika ili watoto wao wapate malezi mema.


Kwenye mahubiri yake, Pasta Tony Kapola alisema kwamba ndoa zilizovunjika husababisha kusambaratika kwa taifa, ikizingatiwa kwamba ni muhimu katika jamii.


Kulingana na Kapola, shida zinazoshuhudiwa katika mataifa tofauti zinaweza kutatuliwa iwapo ndoa zitakuwa thabiti, huku pande zote mbili zikitatua matatizo yanayochipuka. "Familia zetu zikiwa imara, nchi yetu pia itakuwa sawa," pasta huyo alisema.

Kapola aliongeza kusema kila mke na mume ni muhimu sana katika familia, na hivyo basi tatizo lolote halipaswi kuwatenganisha. Akihubiri kwa kupeana mfano katika Bibilia, pasta huyo aliwataka wanaume kuiga mfano wa Joseph aliyeishi na Mary hata ingawa aligundua alikuwa mjamzito bila ya kulala naye. 


Pasta huyo aliwashauri wanandoa kutowasikia watu wanaowashauri kuacha ndoa zao, au kupeana talaka kwa ajili ya shida zilizoko akisema huo sio ushauri mzuri.


"Mungu alimhimiza Yusufu asitoroke. Hakuruhusu Yesi kulelewa na single mother. Siku hizi unashauriwa kuwacha ndoa yako kwa saabu una pesa. Lindeni ndoa zenu na mvumiliane," mhubiri huyo alisema. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo