MTOTO wa umri wa mwaka mmoja amekufa baada ya kutumbukia kwenye ndoo ya maji nyumbani kwao, wakati akicheza.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kihenya wa Kihenya, tukio hilo ni la juzi saa 4:30 asubuhi katika eneo la Buza.
Alisema
mtoto huyo, Najma Omary alikuwa akicheza nje ya nyumba yao kulikokuwa
na ndoo ya maji na alitumbukia kwa kutanguliza kichwa na kunywa maji
mengi yaliyosababisha mauti yake.
Kamanda
Kihenya alisema maiti ya mtoto huyo imehifadhiwa hospitali ya Temeke na
hakuna mtu anayeshikiliwa na Polisi na kwamba uchunguzi zaidi wa tukio
hilo unaendelea kufanywa.
Katika
tukio la pili, watu 14 wamekamatwa na polisi katika mikoa miwili
tofauti ya kipolisi kwa tuhuma za kukutwa na pombe haramu ya gongo
pamoja na misokoto ya bangi.
Kamanda
Kihenya alisema Polisi waliendesha msako juzi asubuhi maeneo ya
Kingungi kwa Nyoka, huko Kiburugwa na kuwakamata watu tisa wakiwa na
bangi puri moja na kete 92.
Watuhumiwa hao wanashikiliwa na watafikishwa mahakamani.
Watuhumiwa hao wanashikiliwa na watafikishwa mahakamani.