Watu 173 wakamatwa kwa ushirikina Rukwa

Jeshi la polisi Mkoa wa Rukwa limewakamata watu 173 wanaojihusisha na vitendo vya kishirikina maarufu lama lambalamba ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za kukomesha vitendo hivyo mkoani humo


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa ACP - Theopista Mallya anasema watuhumiwa 95 walikamatwa katika Wilaya ya Nkasi na watuhumiwa 78 katika Wilaya ya Kalambo 

Inaelezwa kuwa watu hao wamekuwa wakichochea vitendo hivyo vya kishirikina na kusababisha uvunjifu wa amani katika mkoa huo ambapo tayari watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata mtu mmoja akiwa na silaha aina ya Gobole kinyume na sheria, mwingine na Nyara za serikali ambazo ni Ngozi ya Paka Pori na mtuhumiwa mwingine amekamatwa akiwa na vitu ambavyo vinazaniwa kuwa vya wizi zikiwemo TV 3 na Redio Moja.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo