Waganga waonywa kuwapa watoto dawa za mvuto wa kimapenzi


Shirikisho la Waganga wa Tiba za Asili (SHIVYATIATA) Kanda ya Magharibi limesema halitawavumilia wala kuwalinda waganga wa jadi wanaotoa dawa za mvuto wa mapenzi kwa watoto walio chini ya miaka 18.


Akuzungumzia suala hilo Mratibu wa Shirikisho, Athumani Waziri amedai dawa hizo zinazojulikana kwa jina la samba zimekuwa zikisababisha kuwepo kwa ndoa za utotoni na kupelekea watoto kunyanyasika hasa maeneo ya vijijini.

Waziri amefafanua kuwa dawa hizo zina matumizi mengi ikiwamo kutumika katika biashara mbalimbali, hivyo haipaswi kutumiwa na watoto au mtu yeyote ambaye yuko chini ya miaka 18.

“Sisi Shirikisho la Waganga wa Kienyeji tumetoa angalizo kwa mganga yeyote ambaye atabainika kujihusisha na kutoa dawa ya samba kwa watoto wadogo hususani wa kike, tutamchukulia hatua kali za kisheria kwa mujibu wa sheria zetu za shirikisho tulizojiwekea,” amesisitiza Waziri


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo