Wakili adai Sabaya ana tatizo la moyo

Wakili wa Upande wa utetezi katika kesi namba 2 inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya Wakili Helleni Mahuna  ameiambia Mahakama kuwa Sabaya ni mgonjwa na ana tatizo la moyo na kusisitiza kusikilizwa kwa kesi hiyo kwani imekaa muda mrefu


Hakimu Erasto Phili amesema  kesi hiyo imedumu kwa muda mrefu na kuwataka upande wa Jamhuri kama cetifiketi zipo ni vyema zikawasilishwa mahakamani kwani  hakimu mwenye dhamana ya kusikiliza kesi hiyo ambaye ni hakimu Salome Mshasha yupo mafunzoni kwa takribani wiki moja  ili baada ya mafunzo hayo kesi hiyo ipate kusikilizwa


Hakimu phil ameihairisha kesi hiyo mpaka tarehe 21 mwezi wa 11 2022  na mshtakiwa ataendelea kuwa mahabusu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo