Mahakama ya Kisumu nchini Kenya imedumisha kufutwa kazi kwa mwalimu mmoja mkuu wa shule aliyemruhusu mwanafunzi wa kike kumpikia nyumbani kwake.
Mwalimu Mkuu wa shule, Gregory Onyango Obonyo, alikiri makossa kwa mwajiri wake TSC ya kumkubalia mwanafunzi wa kike ambaye alikuwa mgonjwa kupika chakula katika nyumba yake na hata kumpakulia baadhi ya chakula hicho kwenda nacho katika bweni lao.
Katika kile kilichoonekana kama kitendo cha wema kilichorudi na majibu tofauti, mwalimu huyo alidhibitishwa kufutwa kazi na hata ombi lake la kutaka apewe kiasi cha pesa kwa sababu ya kufutwa kwake kufutiliwa mbali.
“Sasa hana kazi - alifutwa kazi na Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) na kufukuzwa kwake kulithibitishwa na Mahakama ya Ajira na Mahusiano ya Kazi mnamo Oktoba 27. Pia, alikuwa amedai fidia ya Shilingi milioni 5.6, nyingi zikiwa takrima. Mahakama, iliyoko Kisumu, ilisema hatakiwi kulipwa senti kwa kushindwa kuthibitisha kwamba ana haki ya kupata takrima; na kwamba atapewa tu cheti cha utumishi,” jarida la Nation liliripoti.
Kazi ya mwalimu hiyo inafika kikomo kwa njia ya utata baada ya kuhudumu kama mwalimu tangu mwaka 1990.
Mahakama ilielezwa kuwa mwanafunzi huyo alipelekwa kwa mwalimu mkoo na walimu wa usimamizi wa bweni ambapo alieleza kuwa alikuwa mgonjwa na alikuwa amelala katika bweni kwa siku mzima.
Mwalimu huyo mkuu alimpa hifadhi katika nyumba yake na kuenda kumtafutia chakula ambacho alimuagiza kukipikia hapo ndani kwake baada ya kumpa dawa na kumruhusu kuondoka kuelekea bwenini na baadhi ya chakula hicho alichopika.