Kijana aliyeokoa manusura wa ajali ya ndege, Kazi Imeanza

NA GODFREY NNKO


MKUU wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali John Masunga amesema, tayari Majaliwa Jackson Samweli amepokelewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji makao makuu jijini Dodoma, SACF Puyo Nzalayaimisi ikiwa ni saa chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kutoa maagizo hayo.

Novemba 7, 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameagiza kijana Majaliwa Jackson Samweli aliyeona ndege ikianguka na kuamua kwenda kutoa msaada wa uokoaji akabidhiwe kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na aingizwe katika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili apate mafunzo zaidi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyasema hayo wakati akiongoza wananchi kuaga miili ya watu 19 waliofariki katika ajali ya ndege ya shirika la ndege la Precision Air katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Ajali ya ndege hiyo aina ya ATR 42-500 yenye namba za usajili 5H-PWF iliyotokea Novemba 6, 2022 asubuhi wakati ikijaribu kutua katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba ikiwa na watu 43 wakiwemo abiria 39, marubani wawili na wahudumu wawili.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo