Wabunge wamchangia Majaliwa Milioni 5

Kijana Majaliwa Jackson aliyehusika kuwaokoa manusura wa ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea Bukoba Mkoani Kagera amefika bungeni leo Novemba 11,2022 na kuchangiwa fedha na wabunge 


Akitangaza kuhusu mchango huo wa hiari uliofanywa na wabunge, Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson amesema kiasi cha fedha kilichopatikana ni Milioni 5 na elfu ishirini na tatu ambazo atakabidhiwa kijana huyo


Spika Tulia amesema kijana Majaliwa anatakiwa kuona cha kufanya kwa wale wenzake katika kuwakumbuka baada ya kupewa fedha hizo kwa kuwa hata yeye aliokolewa wakati akiwaokoa abiria hao wa ndege


Fedha hizo zimekabidhiwa kwa Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Jenista Mhagama ili azikabidhi kwa kijana huyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo