Ajali yatokea Dar, yahusisha magari matatu

Watu kadhaa wanahofiwa kujeruhiwa kutokana na ajali iliyohusisha magari matatu iliyotokea eneo la Kitengule Tegeta jijini Dar es Salaam leo Novemba 11, 2022.


Kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni, Mtatiro Kitinkwi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo alipoulizwa kwa simu, hata hivyo amesema taarifa zaidi atazitoa kwani kwa sasa yupo nje ya ofisi.


“Nilikuwa nje ya ofisi kikazi ndiyo ninarudi, lakini hilo tukio lipo na limetokea…nikirudi ofisi nikiiandaa basi nitatoa taarifa,” amesema kamanda huyo.


Via: Mwananchi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo