Wachumba wa tangu shule ya msingi Wafunga ndoa

Katika wimbo wake wa Meant to Be, Rexha alisema "ikiwa imekusudiwa itakuwa basi itakuwa." Na hakika, ni kweli wanachosema kwamba wakati upendo unakusudiwa kuwa, hakuna kinachoweza kuuzuia.


Kwa Jane na Bwire Jacob, hata kusomea shule tofauti zilizokuwa mbali sio jambo ambalo lingewatenganisha na kuingilia kati ya penzi lao.


Wawili hao walianza kama marafiki wa kawaida tu waliokuwa wakisoma shule moja ya msingi, huku Jacob akimrushia mistari Jane kabla ya usuhuba wao kuchukua mkondo mpya.


Hatimaye, wawili hao walianza kuchumbiana kulingana na ripoti ya My Wedding Uganda. "Tulikutana shuleni. Kwa kweli, tulikuwa naye tangu shule ya msingi hadi hapo darasa la nne, kisha akahamia shule nyingine,” bi harusi alisema. “Lakini alikuwa amerushia ndoano hadi tulipokutana tena chuoni mwaka 2016 tukiwa Makerere. Alikuwa akifanya uhandisi wa ujenzi, lakini nilikuwa nafanya sayansi ya kijamii,' aliongeza.


Wakiwa wamechumbiana kwa zaidi ya miaka mitano, walifanya harusi ya kitamaduni huko Kyenjojo mnamo Julai 2, 2022. Mnamo Novemba 5, wawili hao walikula viapo vya ndoa takatifu katika United Christian Center huko Kasubi, Uganda. 


Katika hadithi nyingine ya harusi yenye kugusa moyo, Theven Raphael na mkewe, Tajera Williams-Raphael, wanaishi maisha ya ndoa yenye furaha miaka mingi baada ya kukutana katika shule ya upili na kuoana miaka sita baadaye. Theven na Tajera walikutana walipokuwa na umri wa miaka 17 katika Shule ya Upili ya Vauxhall huko Kingston, na alijua ndiye, ingawa Tajer hakuwa na uhakika sana.


Kwa kuwa alikuwa na majamaa wengine, Tajera aliwaomba marafiki zake wapigie kura ni nani kati ya wanaume watano waliokuwa wakimtaka ambaye anafaa kuchumbiana naye, na mara kafanya uamuzi wa mwisho, Jamaica Observer iliripoti. "Wakati nilimuona kwa mara ya kwanza, alikuwa na sura ya kupendeza. 


Alikuwa anauza peremende na nikamsihi anipe moja." "Ilikuwa ni mwanzo wa mazungumzo ili niweze kumwomba awe mpenzi wangu. Lakini haikufanya kazi. Hivyo ndivyo nilivyomwomba rafiki yangu ambaye pia alikuwa rafiki yake, namba yake," aliongeza.

Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo