Afisa wa Polisi adondoka Chooni na Kufariki Dunia

Kisanga kilishuhudiwa Jumatano Novemba 16,2022 usiku baada ya afisa wa polisi kuanguka ndani ya choo kaunti ya Homa Bay huko nchini Kenya.

Kennedy Oyoo, ambaye alikuwa kostabo katika kituo cha polisi cha Nyatoto, alianguka ndani ya choo hicho na kufariki dunia. Inaarifiwa kisa hicho kilitokea usiku saa tano wakati alikuwa ameenda haja kwenye choo hicho kilichokuwa kimefurika. Alianguka ndani ya shimo ambapo alipata majera mabaya yanayoshukiwa kusababisha kifo chake.


Mwili wa afisa huyo mwenye miaka 47 ulipatikana Alhamisi Novemba 16 asubuhi hali ambayo imesababisha uzunguzi kuanzishwa. Mkuu wa polisi eneo la Suba Caxton Ndunda alisema choo kilikuwa kimejaa maji na afisa huyo alipata majeraha ya kichwa ambayo huenda yalimfanya kushindwa kuopmba usaidizi. Katika kisa kingine Nakuru, jamaa mmoja yuko kizuizini baada ya kumvamia afande ndani ya kituo cha polisi. Kwenye video ambayo inasambaa mtandaoni, wawili hao wanaonekana wakirushiana makonde mazito ndani ya eneo la kurekodi matukio. 


Afisa aliye na sare rasmi za kazi anaonekana akimwendea raia huyo na kuzungumza naye kabla ya kumlima kofi moja safi. Ni jambo linalomkera jamaa huyo na ghafla bin vuu anamrushia afisa huyo konde moja nzito na kufanya ateguke. 


Maafisa wengine wa polisi pamoja na raia wanakimbia kuokoa hali na kuhakikisha kuwa wawili hao wanaacha kulimana. Kwa mujibu wa jamaa mmoja aliyeshuhudia kisa hicho, mzozo ulizuka wakati wa kurekdoi kisa cha uhalifu. 

Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo