Musukuma amshambulia Bashiru, Wote tuna PHD lakini Simuelewi

Mbunge wa jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku ‘Musukuma’ amemtaka Dr. Bashiru Ally Kakurwa, kujitokeza hadharani na kuomba msamaha kwa kauli alizozitoa hivi karibuni.


Video zinazosambaa mitandaoni, zinamuonesha Dk. Bashiru akihutubia katika Mkutano wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata) ambapo anasikika akitoa matamshi yasiyofaa dhidi ya serikali iliyopo madarakani.
“Nimesikitishwa na kauli ya Dr. Bashiru ambae ni Katibu Mkuu mstaafu wa CCM na imefika mahala ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi na ana heshima ya ubalozi. Sasa kwa maneno ya ujinga aliyo ongea juzi, inabidi na sisi tuchomoe fyuzi kama yeye alivyo chomoa.


"Inauma sana kusikia Rais wako anatukanwa. Kwanza mimi nimekuwa Mbunge hii ni awamu ya pili. Bashiru kanikuta ndani ya Bunge. Nimefanya kazi na Mheshimiwa Magufuli (Marehemu) enzi hizo Bashiru (Dr. Bashiru Ally Kakurwa) akiwa Katibu Mkuu wa Chama.


“Mimi kama Musukuma, namwomba Dr. Bashiru (namweshimu sana) alikuwa Katibu Mkuu wa Chama, wabunge 70 mimi ninawajua, aliwafyekelea mbali na aliwapigia simu na kuwatisha na wanalia mpaka leo, aliwakata majina bila sababu yoyote.


"Tulimsifu sana Magufuli kwasababu alifanya kazi zilionekana; ziliwagusa wananchi na sisi kama viongozi wabunge tulimsemea mazuri, tulimwambia anafanya kazi nzuri na hakuna mtu anapinga; Dr. Bashiru alikuwa kimbelembele kuzungumza mazuri ya Magufuli


“Kama Dr. Bashiru ni msomi kama mimi, ana PhD kama yangu inakuwaje tusimsifu Rais Samia. Ni mradi gani ambao leo umesimama. Anasimama mtu mmoja anakatisha watu tamaa. Haya mazuri yote yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita, nani atakuja kutusemea, Mmarekani?


"Mama (Rais Samia Suluhu Hassan) endelea kufanya kazi, hawa watu kama akina Bashiru wapo tuu; hata Yesu aliwaacha, Mtume Muhammad aliwaacha, Kikwete aliwaacha. Marais wote waliwaacha watu wa namna hii,” amesema Musukuma.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo