Hatimaye Ng’hulimi Ilanga na Katala Kikaja ambao Novemba 16, 2022 Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga ilitengua hukumu ya kifungo cha maisha jela waliyokuwa wamehukumiwa, wamepokelewa kwa shangwe nyumbani kwao, Dutwa, Bariadi mkoani Simiyu.
Wawili hao ambao ni wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), walihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Bariadi kifungo cha maisha jela, baada ya kukutwa na hatia katika makosa ya wizi, unyang'anyi wa kutumia silaha na ubakaji yaliyokuwa yanawakabili.
Wamerejea rasmi nyumbani kwao, na kupokelewa na wananchi wa kata hiyo, wakiwemo wanachama na makada wa Chadema, wazazi, ndugu, jamaa na marafiki ikiwa imepita miaka miwili tangu wakamatwe na kufungwa.
