
Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Dkt Bashiru Ally Kakurwa akihutubia mkutano wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata) uliofanyika juzi mkoani Morogoro, alisema mtandao huo si chombo cha kutoa shukrani kwa yeyote yule, bali ni chombo cha kudai haki na heshima, kauli ambayo imeibua gumzo nchini.
Alisema mtandao huo sio chombo kidogo na kuwataka wanachama wake kuulinda na kuurithisha kwa vizazi vingine kimsimamo, na kwamba wakifikia hatua hiyo, hata changamoto wanazozizungumzia zitapungua.
“(Mviwata) si chombo cha kusifu, si chombo cha kushukuru, tunakushukuru kwa fedha hizi, tunakushukuru kwa kazi hizi, mkianza kazi ya kushukuru kwa haki yenu, hamna maana,” alisema Dk Bashiru ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na Rais.
Tazama Video hapa
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi