Bwana harusi mtarajiwa ajiua siku chache kabla ya kufunga ndoa


Daktari mmoja aliyekuwa akihudumu kwenye zahanati katika Kitongoji cha Saghana wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro amefariki dunia kwa kujinyonga kwa kutumia shuka yake ikiwa zimebaki siku 29 kabla ya kufunga ndoa.


Taarifa kutoka Kijiji cha Makuyni alipokuwa akiishi zinasema Joseph Patrick Ngonyani (33) alijinyonga Novemba 26, siku ambayo alipaswa kwenda ukweni kwake Kijiji cha Lotima nchini Kenya kukamilisha taratibu za mahari.

Mwezi Augosti mwaka huu alimvalisha pete mchumba wake ambapo ndoa alipanga kufunga mwezi Desemba mwaka huu.

Wanaume wengi hufikia hatua ya kujiua kwa kutokuongea, au kuona wakiongea watakua wamejidhalilisha. Please talk to save ur life.

Taarifa ya taasisi ya afya ya akili nchini Marekani (National Institute of Mental Health) inaonesha kuwa 77% ya watu wote wanaojiua ni wanaume. Hizi takwimu zinatisha. Moja ya sababu ya wanaume "kukimbilia" kujiua ni kushindwa kuongea wanapopitia magumu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDMO BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By Peruzibongo