Abiria wanaosafiri kwa basi la Princes Muro lenye nambaya usajili T 551 DPQ lililoondoka Ubungo saa kumi na mbili alfajiri kuelekea Arusha, wamekwama katika kituo cha mafuta cha Kibaha Madafu kuanzia saa moja na nusu asubuhi kwa madai kuwa limeharibika.
Mmoja wa abiria aliyejitambulisha kwa jina la STEVEN HENRY, ameiambia Redio One Stereo kwa njia ya simu kuwa tangu wakati huo hawaoni juhudi za matengenezo na wafanyakazi wa basi hilo akiwemo dereva na kondakta hawajulikani waliko.
Amesema wametoa taarifa ya mkasa huo kituo cha polisi Kibaha na askari wa usalama barabarani waliokwenda eneo la tukio, hawakuwaambia lolote wasafiri hao kuhusu hatua zinazochuliwa aidha zinazowapa au kuwaondolea matumaini ya kuendelea na safari.
