Mvulana wa Miaka 12 Aliyeacha Shule Kumtunza Bibi Mgonjwa, Apata Msaada

Ilikuwa ni wakati wa shangwe kwa wakazi wa mji wa Embu mvulana mdogo akijiunga tena na shule.


Kulingana na Msamaria Mwema, mvulana huyo mdogo aliacha shule ili kumtunza nyanya yake mgonjwa na ndugu zake. Kama kifungua mimba, mvulana huyo alilazimika kuchukua majukumu ya kaka mkubwa na kumtunza bibi yake dhaifu na kaka zake wachanga. “Mamake alifariki dunia miaka sita iliyopita na kuacha watoto wadogo sana, mkubwa ana miaka 12, na alikuja katika shule hii kuanza darasa la 4. Simjui mamake wala babake.


Ndugu zake wawili, wa miaka 10 na tisa, wanapaswa kuwa shuleni lakini wanaweza tu kwenda darasa la 2 kwa sababu hawajawahi fika shule tangu mama yao alipofariki," mwanamke huyo aliambia Standard Digital. 


Alifichua kwamba alikwenda nyumbani kwao walipokuwa wakiishi na kumkuta nyanya yao mpendwa akiwa amedhoofika kimwili Msamaria wema huyo alisema bibi huyo hakuweza kujiinua na alikuwa mgonjwa sana lakini alimpeleka hospitali. 


“Nimekuletea mtoto ambaye ukimwangalia ni kiongozi, nahodha, alivunjika mguu wakati anachota kuni, alijitengeneza magongo mwenyewe, nilimuita daktari apime afya yake na kumnunulia magongo mapya ya kutembea. Nimewasaidia kwa sababu mama hachagui wala hahukumu,” aliongeza. Ukarimu wa mfadhili huyo ulichangamsha mioyo ya wengi mitandaoni na kila mmoja wao alikuwa na maoni yake.


Chanzo:Tuko


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo