Ajiua kwa kunywa maji ya Betri Ludewa

Ni tukio ambalo limetokea wilayani Ludewa mkoani Njombe katika eneo la Ludewa kijijini kanda ya chini ambapo Kijana aliyefahamika kwa jina la Richard Mtafya alimaarufu kama Sumbuko (19) ambaye inasemekana amejiua kwa kunywa maji ya betri ili kukwepa shitaka la mauaji lililokuwa likimkabili .



Mtendaji wa kijiji hicho Athanas Mtega amesema mnamo Novemba 14 mwaka huu kijana huyo kwa kushirikiana na mwenzake walifanya mauaji ya kijana mwenzao aliyefahamika kwa jina moja la Alfred kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

"Sumbuko alikuta sms za Alfred kwenye simu ya mkewe ndipo akamshirikisha rafiki yake na kuchukua jukumu la kwenda kumpiga na kumsababishia umauti, wakati wanatafutwa na polisi Sumbuko alikutwa mahali na kuzingirwa ndipo akaona amekosa mwanya wa kukimbia ikambidi anywe maji ya betri aliyokuwa amebeba kwenye chupa".

Angela Mhagama mkazi wa wilaya ya Ludewa mkoani Njombe ambaye ni mke wa marehemu Richard Mtafya ambaye amejiua kwa kunywa maji ya betri ili kukwepa kesi ya mauaji iliyokuwa ikimkabili ameeleza namna mme wake alivyotekeleza mauaji hayo na kukimbia.


Angela amesema walipeana namba za simu na kijana huyo Alfred aliyeuawa lakini alimuonya asitume ujumbe kwakuwa wanatumia simu moja na mumewe lakini kijana huyo alituma ujumbe ambao mumewe aliuona.


"Mme wangu aliuona huo ujumbe wa Alfred akaniuliza hii ni namba ya nani? Mimi nikamwambia sijui ndo akaanza kuchati nae kisha akaondoka nyumbani na kwenda kutekeleza mauaji"


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo