Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewaonya watunza kumbukumbu nchini kutunza nyaraka za serikali ipasavyo ili zisiendelee kuzagaa mitandanoni kama ilivyo sasa.
Rais Samia ametoa kauli hiyo hii leo Novemba 27, 2022, mkoani Arusha wakati akifungua mkutano mkuu wa 10 wa Chama cha Taaluma ya Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA).
"Kuna mambo tunayaona huko kwenye mitandao, kumbukumbu za serikali ziko mitandaoni, barua sijui nyaraka gani, wale wa mahakamani kesi ilivyohukumiwa, sasa unajiuliza huyu aliyetoa hizi taarifa anataka umaarufu, rushwa au kitu gani!," amesema Rais Samia
Aidha Rais Samia ameongeza kuwa, "Serikali inafanya mambo yake kwa taratibu sasa unapozitoa zile taratibu nje ya utaratibu, hujafanya la maana ndugu yangu niwaombe sana watunza kumbukumbu, sisi wazazi wenu hatukufanya hivyo kwahiyo na nyinyi tunzeni siri za serikali,"