Akili ni nywele kila mtu ana zake waliamba wahenga, katika kaunti ya Kilifi nchini Kenya, wazee wameamua kupaka nywele zao zilizojaa mvi rangi nyeusi ili waonekane vijana.
Idadi ya vifo vya wazee imekuwa ikiongezeka katika siku za hivi karibuni wakimalizwa na vijana wenye tamaa ya kurithi mashamba wanayomiliki. Hivyo, wazee wameamua kujilinda kwa kupaka kanta kwenye mvi zao ili kuwa na mwonekano wa ujana
Kulingana na naibu kamishna wa eneo la Matsangoni, Patience Dama, visa vya urithi ndiyo chanzo cha mauaji ya wazee katika eneo hilo. Dama alisema ameanzisha hamasisho miongoni mwa vijana na wazee kama moja ya jitihada za kupunguza visa hivyo vya mauaji. Kamishna huyo wa polisi alieleza kuwa kulingana na mila na tamaduni za Mijikenda, mtu aliye na umri mkubwa zaidi katika familia ndiye huhifadhi cheti cha umiliki wa ardhi.
Kamishna wa polisi wa kaunti ya Kilifi, Kutswa Olaka naye kwa upande wake alisema wanaotekeleza mauaji hayo wamebadilisha mbinu ya kuuwa. Olaka alieleza kuwa kwa sasa wauaji hao wanawauwa wazee katika njia itakayoenekana kwamba wamejitoa uhai wenyewe kwa kujinyonga. Mzee akatwa seheme zake za siri Katika taarifa tofauti, mzee mwenye umri wa miaka 70, amevamiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana ambao walimkata sehemu zake za siri.
Mzee Uruban Paul, ambaye ni mkazi wa kijiji cha Uru Shimbwe, mkoani Kilimanjaro, Tanzania, alisema alikuwa akitoka kwenda kujisaidia wakati alikutana na watu hao ambao baada ya kumfanyia kitendo hicho walikuwa wakikinga damu yake.
Chanzo: TUKO.co.ke