Polisi katika Eneobunge la Kiminini, kaunti ya Trans Nzoia, wanamsaka kijana mwenye umri wa miaka 21, Brian Wafula, ambaye anashukiwa kumuua mama yake Judith Nafula Konya.
Nafula, ambaye alikuwa akihudumu katika maabara ya Shule ya Wasichana ya St Joseph's Kitale, alitoweka siku ya Jumanne, Oktoba 18, katika hali isiyoeleweka.
Mwili wa marehemu mwenye umri wa miaka 50, baadaye ulipatikana ukielea kwenye Mto Kiminini jioni ya Jumamosi, Oktoba 22. Kabla ya kutoweka kwake, inaripotiwa kuwa Nafula alizozana na mwanawe baada ya kuuza baadhi ya mazao ya shambani bila idhini yake.

Wekesa alisisitiza kuwa mtoto wao ndiye mshukiwa mkuu wa mauaji hayo kwani begi lake lilikuwa na vitu vinavyomhusisha na kifo hicho, zikiwemo funguo za nyumba yao kuu. Wafula anasemekana kutorokea Eldoret.
Chanzo: TUKO.co.ke