Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Suzan Kaganda kuwa Kamishna wa Polisi (CP).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 24, 2022 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, baada ya kumteua, Rais amemteua Kamishna Kaganda kuwa Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu wa Jeshi la Polisi.
Kamishna Kaganda anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi (CP) Benedict Wakulyamba ambaye atapangiwa kazi nyingine ambapo uteuzi huo umeanza mara moja.