MBUNGE mstaafu wa jimbo la Wanging’ombe mkoani Njombe Yono Kevela ametoa wito kwa wananchi wilayani humo kuacha kuchangia michango mikubwa kwa watu wanaooa na kuolewa badala yake waongeze nguvu ya michango kwa watoto ili waweze kupata elimu.
Kevels amesema hayo wakati akizungumza na wananchi akiwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 22 ya kidato cha nne ya shule ya sekondari Ilembula huku akibainisha kuwa baadhi ya vijiji kwenye wilaya hiyo kikiwemo kijiji cha Katenge wamekuwa wakichangia kwa usimamizi wa vijiji vyao hali iliyopelekea kuwa na wasomi wengi wakiwemo madaktari.
“Tuache kuchangia hela nyingi kwa mtu anayekwenda kuoa au kuolewa tuhangaike sasa hivi kwenye swala la elimu,kama mtoto amekosa ada ya kwenda kidato cha tano tuchangishane ili tuwezeshe watoto wakasome,kuna vijiji sasa hivi wana wasomi wengi kutokana na michango yao na wanaletya faida kwa vijiji vyao”amesema Kevela
Vile vile ameomba viongozi wa kisiasa waliopo madarakani kuacha dhana potofu na kushindwa kuwatumia wastaafu kwenye shughuli za maendeleo kwa kuhofia kuondolewa kwenye nafasi zao.