Kamati ya fedha, mipango na Utawala halmashauri ya Wilaya ya Makete ikiongozana na wakuu wa Idara na Vitengo Oktoba 20, 2022 imetembelea mradi wa Ujenzi Kituo cha kuuzia Mazao ya Misitu hususani Mbao (Timber Yard) inayojengwa katika Kata ya Mang'oto
Jackline Mrosso ni Afisa Maendeleo ya jamii Wilaya ya Makete kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya William Makufwe amewaeleza Madiwani ambao ni wajumbe wa Kamati ya fedha mipango na Utawala kwamba mradi huu unatarajiwa kugharimu shilingi Milioni 85, Kati ya fedha hizo Milioni 26 zimetolewa na wafadhili ambao ni Pandamiti Kibiashara na zingine zikitolewa na Halmashauri kupitia mapato ya ndani.