Shamira amesema mwenendo wa maisha ya binti nyumbani hapo uliendelea kumchanganya,kwani wakati mwingine alikuwa akifanya vitu kama mtu asiyekuwa na utimamu wa akili, hatua iliyomfanya kufikia uamuzi wa kutaka kumrudisha nyumbani kwao wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambapo wakati akimwandalia nguo katika begi lake tayari kwa kumsafirisha alikuta tena mchanga na shanga vikiwa vimefungashwa kwenye karatasi.
Kwa upande wake Flora akijibu tuhuma ya ushirikina dhidi yake amesema mchanga na shanga vilivyokutwa ndani ya begi lake aliagizwa na bibi yake ambaye alimtokea kimazingara usiku wa Oktoba 23 mwaka huu, wakati akiangalia runinga sebuleni na kumwambia achote mchanga nje ya nyumba ya familia hiyo na baadaye ataufata bila yeye kujua utakwenda kufanyiwa kazi gani .
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo wa Komba Masai, Dotto Kitungulu, amefika katika nyumba ya familia hiyo ambapo amehakikisha usalama wa binti huyo ambaye alikuwa amezingirwa na wananchi mpaka aliposafirishwa kurudi nyumbani kwao mkoani Shinyanga.