Rais Samia Suluhu Hassan amewaonya viongozi wanaoapa kuitumikia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya kukiuka viapo vyao wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao.
Rais Samia ametoa onyo hilo alipokuwa akiwaapisha mawaziri wapya watatu, Innocent Bashungwa (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), Dkt. Stergomena Tax (Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki) na Angella Kairuki (TAMISEMI).
