Katika kutekeleza adhima ya Mhe Rais Samia Suluh Hassan ambaye ni kiongozi wa machifu nchini Chifu 'Hangaya' ya kuendeleza tamaduni za kichifu nchini, hatimaye Chifu wa kabila la Wanyakyusa, Chifu Edwin Mwakatumbula amekabidhiwa Ikulu yake ya Kichifu na kiongozi wa machifu wadogo wa kabila hilo.
Ikulu hiyo ipo katika Kijiji cha Masoko Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.
Akizungumza katika tukio hilo la kihistoria, Chief Edwin amesema kuwa imekuwa siku ya baraka kwenye himaya hiyo, kwa yeye kukabidhiwa Ikulu hiyo iliyojengwa Mwaka 1,900 huku akiahidi kuendeleza umoja, mila na tamaduni za kabila hilo.
Amesema kuwa aliporithi uchifu wa kabila hilo kutoka kwa marehemu Chifu Daudi B Mwakatumbula miaka 10 iliyopita amejitahidi kuendeleza mila za kabila hizo huku akidumisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa Wanyakyusa wote nchini.
#edwinmoshiupdates