Faini ya Milioni 34.9 kwa Kumgonga Twiga Mikumi

Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi Ignas Gara amesema Dereva wa lori lililomgonga Twiga na kumuua kwenye hifadhi ya Mikumi usiku wa kuamkia September 29,2022 atalipa faini ya dola za kimarekani elfu 15 ambazo ni sawa na shilingi milioni 34 na laki 9.

Taarifa hii imekuja wakati bado Dereva huyo yupo Hospitali akipatiwa matibabu chini ya ulinzi wa Polisi kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye ajali hiyo ambayo lori alilokuwa akiliendesha (T 863 AGU) lilianguka kwa ubavu baada ya kumgonga twiga huyo.
Dereva huyu atakapopona atafikishwa Mahakamani baada pia ya taratibu za kisheria kukamilika.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo