Anayedaiwa kulawiti watoto watatu huyu hapa

Mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Mohamedi Kaisi Hamisi mwenye miaka 47 mkazi wa kijiji cha Kawawa mkoani Mtwara, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za ulawiti.

Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara Lucas Mkondya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kwamba mwanaume huyo anatuhumiwa kulawiti watoto watatu wenye miaka 13, 14 na 15, wa shule ya msingi Kawawa, walipokuwa wanatafuta Nazi kwenye minazi iliyopo vichakani baada ya kutoka shule.

Vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinazidi kushamiri nchini, ambapo hutishiwa na kufanyiwa ukatili huo.

Akizungumzia tukio hilo, kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Lucas Mkondya, amesema watoto waliolawitiwa ni wenye umri chini ya miaka 15 ambapo mtuhumiwa huyo alienda nao porini na kuwatisha kwa panga kabla ya kuwafanyia tukio hilo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo