Madereva wa magari ya serikali waonywa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani , ACP-Jonathan Shanna, amewataka baadhi ya madereva wanaoendesha vyombo vya moto, hasa magari ya Serikali na Viongozi mbalimbali kuacha dhana kua wao wanapaswa kuendesha kwa mwendokasi barabarani .

Kamanda Shanna ametoa hadhari hiyo baada ya kutokea ajali na kusababisha vifo vya watu 3 . Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 9 mchana katika kijiji cha Msolwa, wilaya ya kipolisi Chalinze, ilihusisha  gari la Serikali, chini ya wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji, yenye namba za usajili STK 923 aina ya TOYOTA-LAND CRUISER , iliyokua ikiendeshwa na Bw. Peter mwenye umri wa miaka 23, mkaazi wa Mkoa wa Dar Es Salaam .

Chanzo cha ajali hiyo, kinaelezwa kua ni uzembe wa Dereva aliyekua anaendesha  gari ya Serikali, alipohama upande wake wakati akiyapita magari mengine kwa mwendokasi bila kuchukua tahadhari na kuligonga gari lenye namba za usajili T 920 AQV aina ya SCANIA ,  ambayo dereva wake alitoroka mara tu baada ya ajali .


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo