Watu watatu kati ya sita waliotoweka katika mazingira ya kutatanisha wapatikana

Watu watatu kati ya sita waliotoweka katika mazingira ya kutatanisha usiku wa kuamkia Ijumaa Aprili 6, 2018 katika Kijiji cha Mitambuuni shehia ya Mtambwe, Mkoa wa Kaskazini Pemba wameonekana alfajiri ya leo Jumapili Aprili 8, 2018.
Wameonekana katika Kijiji cha Mkungu Jimbo la Mtambile wilayani Mkoani.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Sheikhan Mohamed Sheikhan amethibitisha kupatikana kwa watu.
Amewataja vijana waliopatikana kuwa ni Said Shanani Mohamed (16), Juma Kombo Fimbo (17) na Abdallah Khamis Abdallah (19).
Imeelezwa vijana hao walionekana alfajiri, wawili kati yao mikononi wakiwa na kamba.
Amesema taarifa zaidi itatolewa baadaye na kamanda wa Mkoa wa Kaskazini ambako ndiko walikotoweka.
“Kwa sasa jeshi linafanya kazi na taarifa rasmi itatolewa kwenu na jamii kwa jumla hapo baadaye,’’amesema kamanda Sheikhan.
Amewataka wananchi kushirikiana na Polisi kwa kutoa taarifa zinazoashiria uhalifu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo