Wanakikundi
cha uhamasishaji cha kata ya Mungaa jimbo la Singida mashariki, wakitoa
burudani kwenye hafla ya uzinduzi wa shina la wakereketwa wa CCM la
Mzambarauni katika kijiji cha Makiungu.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Makiungu
Mjumbe
wa Mkutano Mkuu CCM (NEC) taifa wilaya ya Ikungi mkoani Singida,
Jonathani Njau ameivunja ngome ya CHADEMA kata ya Mungaa, baada ya
wanachama wake 51 kukihama na kurejea CCM.
Wanachama
hao ambao karibu wote ni vijana, katika risala yao wamedai wamehama
CHADEMA, baada ya kubaini kuwa wanatumiwa vibaya na wanasiasa wa chama
hicho.
Wamedai
kwamba wanasiasa wa CHADEMA wamejaa uchu wa madaraka, wanatumia uongo
mkubwa, hila, kupandikiza chuki na wanatoa ahadi za uongo katika kupata
uongozi.
“Kabla
na baada ya uchaguzi, tuliahidiwa ahadi nyingi na viongozi wa CHADEMA
kumbe ahadi zote hizo ni ahadi hewa.Vijana tumekwisha kuwagundua na
hatudanganyiki tena.Kwa sababu sisi ni nguvu kazi ya taifa,tunatakiwa
kutumika kwa maslahi ya taifa na si kwa maslahi ya mtu binafsi”,inasema
sehemu ya risala yao.
Katika
hatua nyingine,vijana hao walishangiliwa kwa nguvu na umati
uliohudhuria mkutano huo wa hadahara,wakati wakiimba wimbo maalum ambao
ulidai kwamba CHADEMA ni sawa na kitanda cha kamba kilichojaa kunguni na
hivyo,hakilaliki.
Akizungumza
muda mfupi baada ya kuzindua shina la wakereketwa la Mzambarauni
waliorejea CCM, Mnec Njau amesema mlango wa CCM upo wazi wakati wote
kupokea wanaCCM waliokimbilia upinzania na kurejea CCM chama pekee
ambacho sera zake zinatelekezeka.
Amesema
hivi sasa kuna wimbi kubwa la wanaCCM waliokimbilia upinzani wanarejea
nyumbani CCM,baada ya kubaini kwenye upinzania na hasa CHADEMA, kumejaa
chuki, uwongo uliopitliza na wananchi wanakatazwa kuchangia maendeleo
yao.
Aidha,
Njau ambaye kitaaluma ni mwanasheria, amewahimiza wakazi wa jimbo la
Singida mashariki kuwapuuza watu/viongozi wanaowadanganya wasichangie
maendeleo yao.
“Kama
tutaendelea kuwaamini wapotoshaji hawa,wilaya ya Ikungi itakuwa tanuru
la kuzalisha vijana/watu bumbumbu hasa kwenye masomo ya sayansi, kwa
sababu hatutaki kuchangia ujenzi wa maabara katika shule zetu za
sekondari za kata”, alifafanua MNEC huyo.
“Katika
karne hii ya sayansi na teknolojia, mtu mwenye akili timamu hawawezi
kugoma kuchangia ujenzi wa vyumba vya maabara,ili mtoto wake aweze
kupata fursa nzuri ya kujisomea masomo ya sayansi kwa ufanisi mkubwa”,
amesema Njau.