Suala la asilimia 20
za mapato ya vijiji limeendelea kuwa gumzo katika baraza la madiwani katika
halmashauri ya wilaya ya Makete kutokana na baadhi ya vijiji kutorejeshewa
asilimia zao
Wakichangia hoja
katika baraza hilo, baadhi ya madiwani akiwemo diwani wa Kinyika Mh Mwalyoyo na
Mh. Beatrice Kyando wameonesha kusikitishwa na halmashauri kuchelewa kulipa
asilimia 20 za vijiji licha ya maagizo kutolewa jambo walilodai linaleta
sintofahamu katika kata zao
Madiwani wengine Mh
Mwipelele Mbogela na Mh Asifiwe Luvanda wakaenda mbali zaidi na kutaka vikao
vya madiwani visitishwe mpaka hapo asilimia 20 za vijiji zitakapolipwa huku
Diwani wa Mlondwe Mh Alphonce akipinga mawazo hayo
Akitoa ufafanuzi wa
hoja hiyo kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mwl. Gregory
Emmanuel amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kusema kwamba kinachopelekea
ucheleweshaji huo ni pamoja na upunguaji wa mapato ya halmashauri jambo
linalopelekea kiasi kidogo kinachopatikana kuelekezwa katika shughuli zingine
zinazohitajika kuendesha halmashauri, huku akikiri kuwa agizo la baraza kutaka
fedha zote za madeni ya asilimia 20 za vijiji zilipwe zote kabla ya Desemba 31
mwaka huu ni ngumu kutekelezeka
Baada ya majadiliano
hayo Mwenyekiti wa halmashauri Mh Egnatio Mtawa akaagiza suala hilo lipelekwe
kwenye kamati ya fedha kujadiliwa na kutoka na mkakati ambao hautaarhiri
uendeshwaji wa shughuli za halmashauri
Sikiliza sauti jinsi ilivyokuwa kwa kubofya play>>>>>>
Sikiliza sauti jinsi ilivyokuwa kwa kubofya play>>>>>>