Rais Magufuli ashindwa kujizuia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameshindwa kujizuia na kuomba kupigiwa kwa mara ya pili wimbo wa msanii wa injili nchini Goodluck Gozbert, uitwao  'Hauwezi Kushindana'

Rais Magufuli ameweka wazi kuwa amevutiwa sana na wimbo huo wakati akiaanza kuhutubia leo April 3, 2018 katika uzinduzi wa mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi 2, ambao unatarajiwa kuingiza megawatts 240 katika gridi ya Taifa.
Baada ya kumaliza kuhutubia Rais Magufuli aliomba wimbo huo upigwe tena na kukiri kuwa amemkosha sana. 
"Naomba niseme tena kale kawimbo kamenigusa sana, naomba kachezwe tena hapa " alisisitiza Rais John Pombe Magufuli 
Msanii Goodluck Gozbert ameachia video ya wimbo wake huu Machi 16, 2018  na kuwagusa watui wengi kutokana na utunzi wake na ujumbe ambao upo ndani ya wimbo huo ambao pia umemguda Rais John Pombe Magufuli.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo