Serikali yasema Ndege Mbili kutua Nchini Julai 4 Mwaka huu

Msemaji mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Hassani Abbasi amesema ndege mbili zipo karibuni kutua nchini ili kufikia idadi ya jumla ya ndege nne ifikapo Julai 4, mwaka huu 2018.
Asubuhi ya Leo tarehe Julai 4, 2018 ameyasema hayo alipofanya mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu serikali ya Tanzania na kuongezea kuwa suala la kushikiliwa kwa ndege aina ya bombadier Q400Dash ni umbea wa watu walio wanafiki na wazandiki waliochomeka maneno.
Lakini amesema kufikia mnamo Julai 4 mwaka huu ndege zote zitakuja ili kuendelea na huduma zake sehemu mbalimbali maana serikali inaendelea na ujenzi wa viwanja zaidi ya kumi nchini ili kukidhi uhaba wa tatizo hilo.
“Serikali inaendelea na upanuzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Juliusi Kambarage Nyerere (JKNIA) katika terminal III na karibuni utakamilika,
Na ujenzi mwingne wa viwanja zaidi ya kumi hapa nchini ili kukidhi uhaba wa viwanja vya ndege”. amesema Dkt. Abbasi.
Serikali imefanya maboresho kwa asilimia 50 katika jengo la abiria la uwanja wa ndege wa songwe na karibuni litafunguliwa, na bado kuna mpango wa kujenga kiwanja kingine kipya cha kimataifa maeneo ya msalato mjini Dodoma. ameendelea kusema.
Kuhusu kukatika kwa umeme na uhaba wa maji katika kipindi hiki Dkt. Abbas amesema kuna changamoto kubwa katika mfumo wa uzalishaji na usafirishaji lakini bado kipo kiwango cha kutosha cha umeme na karibuni tatizo litaisha na ndani ya hii miaka mitatu umeme utauzwa nje ya nchi.
“Serikali inao umeme wa kutosha na katika miaka hii mitatu ni lazima na sisi tuuze umeme nje ya nchi”. amesema Dkt. Abbasi.
Pia amesema kuwepo kwa vilio vingi vya tatizo la maji, hii ni changamoto katika maeneo mengi nchini lakini serikali inaendelea kutatua tatizo hilo.
Aidha Dkt. Hassani Abbasi amesema kwa vile sheria za nchi zinaruhusu uhamishaji wa fedha za maendeleo, wamekuwa wakifanya hivyo ili kutatua matatizo sehemu husika nchini, na fedha kidogo ilizonazo serikali inapambana ili kuyatatua kadri, hivyo amewaomba watanzania kuelewa hivyo.
“Tunapambana na tumeahidi kutatua matatizo mbalimbali nchini kwa fedha kidogo tulizonazo, tunawaomba watanzania watuelewe”. Dkt. Abbas.
Hata hivyo amesema serikali inaendelea na uhakiki wa wadai, ukikamilika wote watalipwa maana pesa ipo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo