Uzalendo wamshinda Padri, Aamua Kufunga Ndoa Rasmi


Miaka tisa baada ya kuvuliwa daraja la upadri wa Kanisa Katoliki, mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii, Privatus Karugendo amefunga ndoa na Rose Birusya.


Ndoa hiyo ilifungwa jana katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini hapa katika misa iliyoongozwa na Padri Stefano Kaombe.

Mapadri wa Kanisa Katoliki hawaruhusiwi kuoa na wanapoachishwa husubiri kibali maalumu kutoka kwa kiongozi wa kanisa hilo duniani.

Akiwa mwenye furaha, Karugendo alizungumza kwa simu na mwandishi wetu kwa dakika chache baada ya kufunga ndoa hiyo.

“Umepata wapi taarifa? Kumbe wamesharusha! Ndiyo tumetoka kanisani tunajiandaa kwenda ukumbini,” alisema Padri Karugendo 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo