Lowassa Ni Moto Wa Kuotea Mbali.....Mamia ya Wachungaji Waandamana Kuelekea Nyumbani Kwake Kumtaka Agombee Urais


Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akimkaribisha mratibu wa msafara wa wachungaji mbalimbali wa Makanisa ya Pentekoste kutoka maeneo mbalimbali nchini, Mchungaji Bernedict Kamzee kutoka kanisa la Glory of Crist la mkoani Katavi. 

Mchungaji Benedickto Kamzee kutoka Kanisa la Glory of Christ la Katavi amesema wamefikia uamuzi huo wa kuja Dodoma kuonana na Edward Lowassa bila kushinikizwa wala kushawishiwa na mtu yeyote.
“Hakuna aliyetushawishi, hata siyo maaskofu wetu, hili suala halina msukumo wowote zaidi ya msukumo wa Mungu,” alisema Kamzee.
Kamzee alisema wachungaji hao wanatoka kwenye madhehebu ya EAGT, TAG, PEFA, KLPT kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza  baada  ya kuwakaribisha  Wachungaji  hao, Lowassa amepinga tuhuma zilizotolewa na baadhi ya watu kwamba amekusanya makundi ya kumuunga mkono huku akidai hana sababu ya kufanya hivyo na hana uwezo wa kuwagharamia watu hao wanao muunga mkono. 
 
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akizungumza na ujumbe huo wa Wachungaji waliofika nyumbani kwake.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Khamis Mgeja akizungumza jambo wakati wa kuwapokea wageni hao.
Wachungaji hao wakiwa nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli mjini Dodoma.
Maombi yalifanyika na Mchungaji Bernedict Kamzee aliwaongoza wachungaji wote katika maombi hayo.
 Maombi yakiendelea

Lowassa akiagana na wachungaji hao leo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo