Akifanya mahojiano na eatv Mh. Kingu amesema kwamba watu wanaoendelea kuzungumzia hoja hiyo ni kama kumkosea heshima Rais wa nchi ambaye yeye ndiyo muhusika wa kuongezewa muda (anayepigiwa chapuo) alishawea wazi nia yake na kusema kwamba hana mpango wa kuongeza muda wa uongozi.
Akizungumzia kuunga mkono hoja hiyo ambayo ilianzihwa na Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia, Mh. Kingu amesema kwamba kwa sasa hoja hiyo si muafaka japo si mbaya kwasababu kwa sasa Rais anachafuliwa sana ikiwepo kupewa majina mbalimbali yasiyo mazuri
Ameongeza kwamba anaamini hata kama mjadala huo utaendelea na kufika ndani ya CCM haitapitishwa kwani hata mazingira yaliyopo siyo rafiki kwa kuupitisha mjadala huo.
"Rais wetu ameshaanza kuchafuliwa sana na hata kupewa majina yasopendeza. Hata kama hoja hii ilikuwa na mashiko, kwa hiki kipindi ikifanyika watu wataanza kusema si tuliwaambia. Kwa kazi anazofanya rais wetu mtu anaweza kutamani labda aongezwe muda lakini naamini hoja hiyo ndani ya CCM haitakubalika. Tukienda mbali zaidi Rais ameshatoa tamko huo mjadala ufungwe, sasa watu wanaoendeleza huu mjadala ni kumkosea Rais heshima, sasa ndani ya chama basi pengine unaweza kuona labda mtu anajipendekeza,". Kingu.
Hata hivyo Kingu ametoa rai kuwa ni vyema kwa sasa watu wakaachana na mjadala huo wa kuongeza miaka na badala yake Katiba ya Tanzania iendelee kuheshimiwa.
Chanzo:EATV