Polisi yakanusha kuwaona mashekhe waliokuwa wametekwa

Jeshi la Polisi Zanzibar limesema kuwa halina taarifa za kuonekana kwa mashekhe watatu wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, ambao waliripotiwa kutoonekana tangu Januari 9, mwaka huu

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali, alisema jeshi hilo lilifanya kazi ya kuwatafuta mashekhe hao, lakini halikufanikiwa kuwaona. 
“Zipo taarifa mitaani kuwa mashekhe hao wameonekana sasa nashangaa kwanini waliokuja kuripoti kuwa hawaonekani wameshindwa kuja kutoa taarifa kuwa wameonekana,” amesema. 
Kamanda huyo ameiasa jamii kuacha kuchanganya mambo ya kihalifu na kisiasa kwa kuwa halileti taswira nzuri kwa jamii na taifa kwa ujumla. 
Ameongeza kwamba awali jeshi hilo lilipokea taarifa rasmi kutoka kwa familia na ndugu wa mashekhe hao, kuwa hawaonekani na wamepotea katika mazingira ya kutatanisha huku likihusishwa jeshi hilo kuwa ndio lililo wachukua.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo