Mwalimu wa shule ya sekondari ya Nyakisasa iliyopo mkoani Kagera aliyetambulika kwa majina ya Deogratias Simon anashikiliwa na jeshi la polisi Kagera kwa tuhuma za kumkashfu Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Mwalimu huyo anadaiwa kutenda kosa hilo mwaka 2016 kupitia mitandao ya kijamii ambapo inadaiwa alikuwa akisambaza ujumbe ambao polisi wanaona ulikuwa na lengo la kumchafua Rais Magufuli.
Jeshi la polisi Kagera litamfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo baada ya uchunguzi kukamilika ili kumshtaki kwa kosa hilo analodaiwa kulifanya mwaka 2016.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi