Wajumbe wa serikali ya Kijiji cha Tandala wilayani Makete mkoani Njombe watapimwa kilevi kabla ya kuingia kwenye kikao ili kuwabaini wajumbe wanaokunywa pombe na kuingia kwenye kikao ilihali sheria hairuhusu, kwa kuwa jeshi la polisi limetaarifiwa na kinachosubiriwa ni makubaliano ya hilo
Hayo yamesemwa na Afisa mtendaji wa Kijiji Hicho Robert Nnko katika kikao cha serikali ya kijiji hii leo, na hiyo ietokana na operesheni waliyoiendesha jana ya kupambana na wale wanaokunywa pombe muda wa kazi, ambapo katika operesheni hiyo baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji walikamatwa wakinywa pombe kilabuni muda usioruhusiwa kisheria
Mtazame katika video hii hapa chini:-
