Madaktari waliofanya upasuaji wa kichwa kwa mgonjwa asiyestahili wasimamishwa kazi

Madaktari(baadhi) Hospitali ya Kenyatta wamesimamishwa kazi kwa kufanya upasuaji wa kichwa kwa mgonjwa asiyestahili.
Picha sio ya tukio halisii
Walibaini kosa hilo wakiwa tayari wamempasua mgonjwa huyo na kugundua hakuwa na tatizo la kuvilia damu walilotakiwa kulitibu
Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Lily Tare, amevieleza vyombo vya habari ya kuwa kulikuwa na wagonjwa wawili, mmoja ndiye aliyetakiwa kufanyiwa upasuaji wa kichwa kwani alikuwa na damu iliyovimba ndani ya kichwa.
Tare ameeleza kuwa waliohusika na kwa sasa tayari wanafanyiwa uchunguzi kupitia sakata hilo ambao ni daktari wa upasuaji wa ubongo, muuguzi, na mtalaamu wa dawa za usingizi.
Hatahivyo ameomba radhi na kueleza kuwa mgonjwa halisi aliyekuwa anatakiwa kupasuliwa kichwa tayari ameshafanyiwa upasuaji huo na afya yake tayari imeanza kuimarika.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo