Akamatwa kwa kumchoma moto baba yake

Jeshi la Polisi huko Bomet nchini Kenya, linamshikilia kijana mmoja kwa tuhuma za kumchoma moto baba yake mzazi

Polisi wa eneo hilo wamesema mzee huyo alikwenda kwenye duka la familia ambako mtoto wake huyo yupo na kula vitafunwa, na alipotoka kijana wake alimfuata na kumwagia mafuta ambayo yanaaminiwa ni petroli na kumuwasha moto.
“Baba mtu alipoenda kupata vitafunwa, mmiliki wa duka alimfuata na kumwagia mafuta ambayo tunaamini ni petroli na kumchoma moto”, amesema mkuu wa polisi wa eneo hilo la Bomet, Samson Rukunga.
Mzee huyo aliyechomwa moto amekimbizwa kwenye hospitali ya misheni ya Tenwek ambako anapatiwa matibabu, kutokana na kupata majeraha makubwa ya moto.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo